Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia tawi lake la Hindiyya imefanya nadwa iitwayo (nafasi ya shahidi katika Quráni tukufu), mtoa mada alikuwa Shekh Wasam Abudi katika moja ya kumbi zilizopo kwenye jengo la Qaaimu hapa wilayani.
Nadwa imefunguliwa kwa Quráni tukufu, na kuhudhuriwa na viongozi wa kidini na kijamii wakiongozwa na mkuu wa wilaya Ustadh Muntadhiru Shafi, baada ya kusomwa Quráni ya ufunguzi ukafuata mhadhara ambao mambo tofauti yameelezwa, ikiwa ni pamoja na ukubwa wa daraja la shahidi huko akhera, na utukufu wake unaoshinda viumbe wote duniani, kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu ndio utukufu mkubwa zaidi, huku akitoa ushahidi wa aya za Quráni, sambamba na kukumbusha mashahidi wema waliotangulia katika historia kwa mfano (Hamza bun Abdulmutwalib, Jafari Twayaar na Imamu Hussein –a.s-), akahitimisha kwa kuwataja mashahidi wa Iraq walio pigania taifa hili na kulinda maeneo matakatifu dhidi ya magaidi wa Daesh, pale walipo itikia wito wa fatwa takatifu ya kujilinda iliyo tolewa na Marjaa Dini mkuu.
Akamalizia mhadhara wake kwa kumkumbuka mmoja wa mashahidi wa fatwa ya kujilinda, aliye uwawa katika vita ya kulinda taifa la Iraq na maeneo matakatifu, na hapo familia ya shahidi Maitham Abdulhadi ikapewa zawadi.