Kufungua mlango wa kupokea wahitimu wa shahada ya masta katika tiba ya meno

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza nafasi ya kazi kwa wahitimu wa shahada ya masta walio somea mambo yafuatayo:

  • 1- Kutengeneza meno.
  • 2- Kutibu meno ya watoto.
  • 3- Kutibu meno kwa kuyakinga.

Chuo kimeweka sharti kwa muombaji awe tayali kufanya kazi muda wote chuoni, waombaji watapewa mtihani wa majaribio kwa kufuata viwango vinavyo kubaliwa na chuo.

Muda wa kutuma maombi ni kuanzia tarehe (7/ 12/ 2020m) hadi (16/ 12/ 2020m), kwa kila anayetaka kutuma maombi afike kwenye jengo la chuo lililopo Najafu Ashrafu –mtaa wa Nidaa- nguzo namba 23 karibu na jengo la makazi la Amiraat akiwa na vitu vifuatavyo:

  • 1- Maelezo yake binafsi (CV).
  • 2- Shahada ya chuo.
  • 3- Vitambulisho vyake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: