Daru Rasuul Aádham (s.a.w.w) imetangaza kurefusha muda wa kufanya kongamano lake la kimataifa

Maoni katika picha
Daru Rasuul Aádham (s.a.w.w) katika kituo cha (Al-Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat) chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kurefusha muda wa kufanya kongamano lake la kielimu na kimataifa la pili kuhusu historia ya Mtume (s.a.w.w), litakalo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu anasoma nyaraka takasifu) chini ya anuani isemayo: (historia ya Mtume katika mtazamo wa Quráni tukufu na riwaya sahihi) hadi mwezi (15 – 16 Rabiul-Awwal 1443h) sawa na tarehe (21 – 22 Oktoba 2021m) kutokana na kuwepo kwa janga la Korona.

Mada za kongamano zitakuwa kama zifuatavyo:

Mada ya kwanza: Historia ya Mtume kabla ya Biítha katika mtazamo wa Quráni tukufu na riwaya sahihi.

  • - Wazazi wa Mtume (s.a.w.w).
  • - Kubashiriwa kwa Utume wa Muhammad (s.a.w.w).
  • - Utoto wa Mtume (s.a.w.w).
  • - Kunyonya kwa Mtume (s.a.w.w).
  • - Kulelewa kwa Mtume (s.a.w.w).
  • - Sifa zake na tabia zake (s.a.w.w).
  • - Kuoa kwa Mtume (s.a.w.w).
  • - Mambo yaliyotokea kwa Mtume (s.a.w.w) baina ya karama na batili.
  • - Kutojua kusoma na kuandika kwa Mtume (s.a.w.w).
  • - Umaasumu wa Mtume (s.a.w.w).

Mada ya pili: Historia ya Mtume mtukufu baada ya Biítha katika mtazamo wa Quráni tukufu na riwaya sahihi.

  • - Kutumwa kwa Mtume.
  • -
  • - Mtume (s.a.w.w) na jamii ya watu wa Makka.
  • - Kuongea kwa Mtume (s.a.w.w) na hoja zake.
  • - Kuhama kwa Mtume.
  • - Mafanikio ya Mtume (s.a.w.w) (kujenga msikiti, kuunga undugu, mkataba).
  • - Sheria za faradhi na hukumu.
  • - Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s).
  • - Mtume (s.a.w.w) na wake zake.
  • - Mtume (s.a.w.w) na maswahaba wake.
  • - Wilaya na Uimamu.
  • - Mtume (s.a.w.w) na washairi.

Mada ya tatu: Vita za Mtume (s.a.w.w) katika mtazamo wa Quráni tukufu na riwaya sahihi:

  • - . sababu zake na matokeo yake.
  • - Mafuhumu ya jihadi na amani ya nchi.
  • - Wasia wa Mtume (s.a.w.w) kwa wajumbe wake.
  • - Imamu Ali (a.s) na vita za Mtume (s.a.w.w).
  • - Ngawira, mateka na fidia.
  • - Mikakati ya kijeshi.
  • - Mtume (s.a.w.w) kuomba ushauri kwa maswahaba zake.

Masharti ya kushiriki ni:

  • 1- Kuzingatia lengo la kongamano, msingi wa tafiti utokane na aya za Quráni pamoja na riwaya sahihi.
  • 2- Mada ziandikwe kwa lugha mbili kiarabu na kiengereza.
  • 3- Utafiti usiwe umeshawahi kutolewa au kutangazwa.
  • 4- Utafiti ukamilishe vigezo vya kielimu, uzingatie misingi ya kielimu katika uandishi na utoaji wa shuhuda za mapokeo.
  • 5- Tafiti zitawasilishwa kwenye kamati ya majaji, kamati hiyo haiwajibiki kurudisha tafiti kwa muhusika iwapo itakosa vigezo.
  • 6- Tafiti iandikwe kwenye karatasi ya (A4) kwa hati yenye ukubwa wa saizi (16) na kutunzwa kwenye (cd) na isizidi kurasa (30).
  • 7- Utafiti uzingatie mada tulizotaja, mshiriki anatakiwa kuchagua mada moja.
  • 8- Utumwe muhtasari wa tafiti katika Ataba mbili tukufu kwa lugha ya kiarabu na kiengereza, pamoja na jina la muandishi na anuani yake sambamba na namba ya simu na barua pepe, haitakiwi kuzidi maneno (500) katika muhtasari huo.
  • 9- Tutaanza kupokea mihtasari tarehe 1/12/2020m.
  • 10- Mwisho wa kupokea mihtasari ni tarehe 1/8/2021m.
  • 11- Tafiti zitumwe kwenye anuani ya barua pepe ifuatayo: daralrasoul313@gmail.com
  • 12- Atabatu Abbasiyya tukufu itagharamia usafiri na malazi ya wageni kutoka nje ya Iraq, pamoja na kuwapa haki zote za ugeni watafiti kutoka ndani ya Iraq (kongamano litafanywa kulingana na mazingira ya afya ya wakati huo).
  • 13- Tafiti zitakazo faulu zitaandikwa kwenye toleo maalum la matukio ya kongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: