Kituo cha turathi za Karbala kimemaliza semina ya (faharasi ya kiufundi) iliyo tolewa kwa watumishi wake wa idara ya uhakiki, kwa ajili ya kuongeza uwezo wao katika sekta hiyo.
Semina imedumu kwa muda wa wiki mbili, chini ya mkufunzi Ustadh Mustwafa Hamdani, ambaye amefundisha misingi na zana za elimu ya faharasi, na ulazima wa faharasi ya kitaalamu, amefundisha kwa nadhariya na vitendo.
Malengo ya semina ni kuwafanya wadau wa faharasi waingie katika uwanja wa kutafakari na kufanya kazi kwa ufanisi na wawe waelekezaji wa wenzao katika fani hii.
Tambua kuwa idara ya kituo cha turathi za Karbala, inajitahidi kuwapa watumishi wake semina zaidi katika siku zijazo, kwa ajili ya kuongeza uwezo wao.
Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ni moja ya vituo vilivyo jikita katika kuhuisha turathi za Karbala, kimefanikiwa kutoa machapisho na vitabu muhimu na bado kinaendelea kuandika hadi sasa.