Mradi wa ujenzi wa kituo cha kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Al-Ameed umepiga hatua kubwa

Maoni katika picha
Kitengo cha majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimesema kuwa ujenzi wa mradi wa jengo la wanafunzi wa jiba ya meno katika chuo kikuu cha Al-Ameed, kilichopo kitongoji cha Saádiyya katika mkoa wa Karbala upo katika hatua za mwisho, umesha kamilika kwa asilimia %90 na kazi bado inaendelea, tunatarajia kukamilisha ujenzi ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora mkubwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mhandisi mkazi Karari Barihi, amesema: “Jengo hili litakua la mfano katika vituo vya kufundishia hapa Iraq, linajengwa kisasa zaidi kwa ajili ya kutumika kufundishia wanafunzi wa udaktari wa meno, sambamba na kuweka vifaa-tiba vya kisasa”.

Akabainisha: “Jengo linaukubwa wa mita (240) lina ghorofa nne (ya chini na tatu za juu) ghofora ya chini inavyumba vitatu vya ofisi ya jengo na mapokezi pamoja na vyumba vingine vitatu, ghorofa tatu zingine kila moja inakumbi mbili na vyumba viwili vya mapokezi, kila ukumbi unaingia wanafunzi (28) kwa kuzingatia eneo maalum la kila mmoja, likiwa limewekwa vifaa vyote vinavyo hitajika, aidha kuna sehemu ya vyoo inayo jitegemea”.

Akaendelea kusema: “Jengo linangazi ya umeme na linawekwa viyoyozi vya kisasa, vifaa vya zimamoto na mfumo wa maji na mawasiliano, mbinu za kisasa za kiusalama zimetumika sawa na majengo mengine ya aina hiyo”.

Akamaliza kwa kusema: “Kilicho baki katika ujenzi ni hatua za kumalizia kupiga ripu kuskimu ukuta na kupaka rangi nje na ndani, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu jengo litakua tayali kwa matumizi mwanzoni mwa mwaka wa masomo ujao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: