Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kushiriki kwenye maonyesho ya kimataifa na kuwa kituo chake cha kwanza cha maonyesho ya vitabu ya kimataifa hapa Iraq

Maoni katika picha
Arabatu Abbasiyya imeanza kushiriki kwenye maonyesho ya kimataifa, baada ya kusimama kwa muda kutokana na janga la viruri vya Korona, leo inashiriki kwenye maonyesho ya kwanza baada ya kusimama kwa muda, ushiriki huu ndio mwanzo wa kuendelea kushiri kwenye maonyesho mengine ya kimataifa, maonyesho haya ya vitabu awamu ya kumi hapa Iraq, yameandaliwa na taasisi ya habari utamaduni na ufundi, yameanza siku ya Jumatano (9 Desemba 2020) na yataendelea hadi tarehe kumi na tisa mwezi huo, jumla ya taasisi za usambazaji wa vitabu (300) zimeshiriki kutoka nchi (21) za kiarabu na kiajemi.

Bendera ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye maonyeho haya imepeperushwa na kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, zikiwa na machapisho tofauti ya kidini na kitamaduni, pamoja na kuonyesha kazi za kiufundi, kiongozi wa idara ya maonyesho Sayyid Muhammad Aáraji ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ushiriki huu ni sehemu ya kuendeleza ushiriki uliotangulia, utofauti wa machapisho na vitabu tulivyo navyo ndio sifa kubwa tuliyo nayo kwenye maonyesho haya, ambayo zaidi ya nakala (300) za matoleo tofauti ya vitabu zimeshiriki, zote nimetokana na kazi halisi ya Atabatu Abbasiyya kuanzia kuandika hadi kuchapisha, hii ndio tofauti kubwa ya matawi yetu na matawi mengine”.

Akasisitiza kuwa: “Tunatarajia ushiriki wa maonyesho haya yanayo fanywa katika mazingira ya pekee yawe muendelezo wa mafanikio yaliyo patikana katika maonyesho mengine, nalo ni dirisha muhimu ambalo Atabatu Abbasiyya hulitumia kufikia jamii inayo izunguka, kazi nyingi zinazo onyeshwa ni zile za kitamaduni na harakati za kielimu zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, zimeonyesha mafanikio mazuri yaliyopo katika Ataba tukufu, katika sekta ya utamaduni, elimu na turathi”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi kwenye maonyesho ya kimataifa yanayo fanywa Bagdad, ambayo huyachukulia kuwa maonyesho muhimu kwake, sambamba na kushiriki kwenye maonyesho na makongamano mengine ndani na nje ya Iraq, yanayo endana na mkakati wake wa kueneza fikra na mafundisho ya Ahlulbait (a.s), matawi yake yamepata muitikio mkubwa kutoka kwa wageni wanaotembelea maonyesho haya, kwa sababu ya kuwa na vitabu vingi tofauti na maonyesho yaliyo pita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: