Ufunguzi wa kituo cha kusaidia na kuelekeza wanafunzi wanaopenda kujiunga na chuo cha Alkafeel

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefungua kituo cha kusaidia na kuelekeza wanafunzi wanaopenda kujiunga katika vitivo vyake (udaktari wa meno, famasia, teknolojia ya udaktari, kitengo cha maabara, uhandisi na teknolojia, kitengo cha uhandisi na teknolojia ya kompyuta, sheria) kwa mwaka wa masomo (2020/ 2021), kwenye majengo ya chuo katika mkoa wa Najafu/ barabara ya (Najafu – Karbala)/ mkabala na nguzo namba 23/ mtaa wa Nidaa/ jirani na nyumba za makazi Amiraat.

Rais wa kituo Dokta Haidari Abudi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ufunguzi wa kituo hiku umetokana na maelekezo ya rais wa chuo Dokta Nuris Muhammad Shahidi Dahani, kwa ajili ya kurahisisha usajili wa wanafunzi chini ya maelekezo yaliyo tolewa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, kituo kinakamati kadhaa, ambazo ni: (kamati ya mapokezi, kamati ya usajili, kamati ya usajili kwa njia ya mtandao na kamati ya uhakiki), zinapokea wanafunzi na kuwaelekeza pamoja na kujibu maswali yao”.

Akaongeza kuwa: “Kituo kinapokea wanafunzi na wazazi au walezi wao kila siku katika siku za wiki, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, kituo kimechukua hatua za kujikinga na maambukizi, ikiwa ni pamoja na kusimamia umbali unaokubalika kiafya kati ya mtu na mtu, kupuliza dawa na kuvaa barakoa”.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kimesajiliwa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, kwa namba (J/H/S 187 1/2/2005).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: