Taasisi ya kimataifa ya Nidaa Jiniva imepongeza kazi za kibinaadamu zinazo fanywa na kikosi cha Abbasi na wamekubaliana kufanya warsha ya sheria za kimataifa na kibinaadamu

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji liwaau/26 Hashdu-Shaábi kimefanya makubaliano na taasisi ya kimataifa ya Nidaa Jiniva, kufanya warsha ya pamoja inayo husu sheria za kimataifa na kibinaadamu na kuzifafanua ili zieleweke zaidi.

Makubaliano hayo yamefanyika baada ya kiongozi wa taasisi hiyo Ustadh Muwafaq Khafaji kutembelea ofisi za kikosi cha Abbasi katika mkoa mtukufu wa Karbala na kukutana na kiongozi mkuu wa kikosi hicho Maitham Zaidi, Khafaji amepongeza kazi za kibinaadamu zilizofanywa na kikosi cha Abbasi wakati wa vita ya ukombozi, hususa katika kulinda wakimbizi na kuandaa sehemu salama kwao, pamoja na kuwapatia mahitaji ya lazima kwao kama vile chakula na huduma za matibabu, sasa hivi kikosi hicho kinaendelea na vita ya kupambana na virusi vya Korona, kwa kutoa mafunzo mbalimbali, kupuliza dawa, na kusambaza vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.

Mwishoni mwa kikao hicho Khafaji akasema: “Leo tulikua na kikao chenye faida kubwa pamoja na viongozi wa kikosi cha Abbasi, tumejadili sekta za ushirikiano sambamba na kufundisha sheria za kimataifa na kibinaadamu, na kulinda raia na mali zao, na kulipa umuhimu wa pekee swala la kuhudumia wakimbizi kwa kuwapa mahitaji ya lazima pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama”.

Akasema: “Tumekubaliana kufanya warsha kuhusu sheria za kimataifa na kibinaadamu, chini ya wawezeshaji wa kimataifa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: