Maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni maktaba pekee hapa Iraq iliyo tekeleza lengo la tifa katika malengo ya umoja wa mataifa ya maendeleo endelevu (SDG)

Maoni katika picha
Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kitengo cha habari na utamaduni, imetekeleza lengo la tisa katika malengo ya maendeleo endelevu, kutokana na ripoti ya mwisho iliyotolewa na umoja wa mataifa kwa jumuiya na taasisi yenye anuani isemayo: (Maktaba za (IFLA) zilizo tekeleza malengo ya maendeleo endelevu katika mazingira ya janga la Korona).

Ustadh Ammaar Hussein Jawadi mkuu wa kituo cha taaluma za namba ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ripoti imetaja nafasi ya maktaba duniani katika kutekeleza malengo kumi na saba katika malengo ya maendeleo endelevu (SDG) wakati wa mazingira ya janga la Korona, yaliyo sababisha kuwe na ugumu wa kutekeleza malengo hayo”.

Akafafanua kuwa: “Umoja wa maktaba na taaluma (IFLA) wenye wanachama katika nchi (150) umeandaa ripoti, inayo tokana na taarifa walizo kusanya kutoka kwenye maktaba wanachama kila sehemu ya dunia wakati wa janga la virusi vya Korona, maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefanikiwa kutekeleza lengo la tisa katika malengo ya maendeleo endelevu (viwanda, ujenzi na tehama), maktaba imeendelea kutoa huduma kwa kutumia Tehama, kama vile kuazima vitabu ukiwa mbali (Lending Service) iliyokua ikitolewa na kituo cha taaluma za namba chini ya maktaba”.

Akaongeza kuwa: “Kutokana na huduma hiyo ambayo ilitufanya kuwa wa pekee hapa Iraq, tumeingizwa katika ripoti ya umoja wa mataifa na tunafurahi kuona maktaba yetu ndio inayowakilisha taifa la Iraq kwenye umoja muhimu wa (IFLA) unao angalia maslahi ya maktaba na vituo vya elimu, kwa kufanikiwa kwetu kutekeleza lengo la tisa katika malengo ya maendeleo endelevu kupitia huduma zinazo tolewa na kituo, maktaba yetu inakua maktaba pekee iliyo tekeleza rasmi malengo ya mpango wa maendeleo endelevu 2030 ya umoja wa mataifa”.

Akaendelea kusema: “Huduma hii inalenga kuwapa watafiti machapisho ya elimu kwa kutumia anuani za barua pepe zao bure, baada ya kujaza fomu maalum, baada ya kufungwa maktaba kutokana na janga la Korona, tuliamua kutumia njia hiyo kwa ajili ya kuwasaidia watafiti wa Iraq, ambapo waliweza kupokea machapisho na vitabu mbalimbali wakiwa majumbani mwao”.

Tambua kuwa kutokana na muitikio mkubwa wa wasomi wa kiiraq, waliojitokeza kuazima vitabu kwa njia ta mtandao, kituo kililazimika kuanzisha mtandao rasmi kwa kazi hiyo, tunaendelea kuongeza vipengele vya mwisho kwenye mtandao huo, na kuwa na mtandao bora unaokidhi mahitaji ya wasomi wa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: