Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu asubuhi ya Jumapili ya mwezi (27 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (13 Desemba 2020m) kimefungua semina iitwayo (Tafiti za kielimu) chini ya ukufunzi wa mwalimu wa hiatoria katika chuo kikuu cha Karbala Dokta Ali Twahiri Alhilliy kwa wafanyakazi wa kituo, kwa ajili ya kuongeza uwezo wao wa kufanya tafiti, semina itaendelea kwa muda wa siku saba.
Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo Dokta Ihsanu Algharifi: “Watafundishwa vitu mbalimbali kuhusu hatua za kuandika tafiti za kielimu kwa mujibu wa mtazamo wa kisekula, tunaamini semina hii itakua na matokeo muhimu kwa wahusika, kwani wapo katika uwanja wa kufanya hakiki na kuandika tafiti”.
Akaongeza kuwa: “Tumechagua mada hii kutokana na ukweli kuwa ni muhimu kutambua hatua za msingi unazo takiwa kufuata katika kuandika tafiti, zinazo kubalika na wataalamu wa kisekula, mfumo wa kuandika tafiti za kielimu unakanuni nyingi hivyo ni muhimu kwa kila mtafiti na muandishi kujiendeleza kielimu”.
Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Karbala kimeandaa mfumo wa kuwaendeleza watumishi wake, ikiwa ni mapoja na kuwapa semina na warsha za ndani na nje kulingana na fani ya kila mtumishi, ili kuboresha kiwango chao cha elimu na utendaji.