Kazi ya kutengeneza Maqaam ya mkono wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wa kushoto imekamilika kwa asilimia %80

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango yake mitukufu chini ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Naadhim Ghurabi amesema kuwa: utengenezaji wa dirisha la Maqaam ya mkono wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wa kushoto, imekamilika kwa asilimia %80 na bado kazi inaendelea, kazi inaenda kama ilivyo pangwa.

Akaongeza kuwa: “Watumishi wa kitengo pamoja na kuwa na kazi nyingi za kutekeleza miradi mingine, ukiwemo mradi wa kutengeneza dirisha la bibi Zainabu (a.s), kazi inaendelea katika maeneo mbalimbali, dirisha hili litakua na uzuri wa pekee unao endana na hadhi ya mwenye nalo”.

Akabainisha kuwa: “Tumesha maliza kutengeneza na kuweka vipande vyote vya dirisha vipatavyo nane, kila kimoja kina ukubwa wa (sm 190) na upana wa (mt 1), ukiwemo mlango wa dirisha ambao imebaki sehemu ya mbele peke yake”.

Akaendelea kusema: “Hali kadhalika tumemaliza kutengeneza nguzo za pembeni zinazo beba vipande vya dirisha tulivyo sema, zipatazo (16) zenye urefu wa (sm 98) aidha tumekamilisha kutengeneza sehemu ya chini yenye mapambo inayo beba (taji la nguzo)”.

Akasema: “Miongoni mwa sehemu muhimu inayo karibia kukamilika ni nguzo za msingi zipatazo (8), zinazo zunguka dirisha pande zote, urefu wa nguzo moja ni (sm 154), zina nakshi na mapambo pia ni imara”.

Akasisitiza kuwa: “Kazi inaendelea ya kuweka urembo wa mwishomwisho (ufito uliotiwa dhahabu) unao zunguka kwenye vipande vyote nane vya dirisha, pamoja na kuendelea kuandika herufi za Quráni (maandishi ya Quráni) na mstari wa mashairi (maandishi ya mashairi), yaliyotiwa maji ya dhahabu na mina ya kijani, yanayo zunguka dirisha pande zote, pia kazi hiyo ipo katika hatua za mwisho”.

Kuhusu kazi ya ndani ya dirisha amesema kuwa: “Ndani ya dirisha kuna mbao za kienyeji za swaghi zilizo wekwa nakshi na mapambo yenye rangi nzuri, mbao nzuri na imara zaidi, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kazi hiyo pia imesha kamilika”.

Kumbuka kuwa dirisha la pembe nane ndio la kwanza kutengenezwa kwa muundo huo, linamzunguko wa (mt 3) na urefu wa (mt 2.85), limetengenezwa kwa silva ya ujazo wa (ml 2), limesanifiwa na kutengenezwa kwa umakini mkubwa na ubora wa hali ya juu, na kazi hii kuingizwa katika orodha ya mafanikio mengi yaliyopatikana ndani na nje ya Iraq kupitia mikono ya raia wazalendo wa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: