Sayyid Alaa Mussawi asifu kazi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kufundisha elimu ya dini ya kiislamu na kulinda misingi sahihi

Maoni katika picha
Rais wa wakfu Shia wa zamani Mheshimiwa Sayyid Alaa Mussawi amesifu kazi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kueneza elimu ya Dini ya kiislamu na kulinda misingi sahihi na fikra za Ahlulbait (a.s) kupitia kushiriki kwake kwenye harakati tofauti za kielimu yakiwemo maonyesho ya vitabu ya kimataifa hapa Iraq yanayo fanyika hivi sasa.

Ameyasema hayo alipo tembelea tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki katika maonyesho, na akasikiliza kuhusu harakati za kielimu na utamaduni zinazo fanywa na tawi hilo, kupitia kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, vitengo ambavyo vimepata mwitikio mkubwa kwenye maonyesho hayo, kila aliyetembelea tawi hilo amesifu ujumbe mwema unaotolewa unaotokana na mafundisho ya Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Kumbuka kuwa kushiriki kwenye maonyesho haya ni muendelezo wa ushiriki wa maonyesho mengine, aina mbalimbali za machapisho wanayo onyesha, ambayo ni zaidi ya aina (300), yote yametokana na kazi halisi ya Ataba tukufu, kuanzia uandishi hadi uchapishaji, nayo ndio sifa ya pekee kwa tawi hili ukilinganisha na matawi mengine, machapisho yake yanadhihirisha ukubwa wa kazi inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya elimu utamaduni na turathi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: