Maahadi ya Quráni tukufu inafanya ratiba ya kila wiki ya (Visa bora)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kupitia tawi lake la mkoani Najafu, imeanza kufanya ratiba ya kila wiki ya (visa bora), nayo ni ratiba ya tafsiri, kila wiki unatolewa mhadhara mmoja, ndani ya moja ya kumbi za tawi hilo na kuhudhuriwa na kundi la wadao wa Quráni kwa idadi maalum kama itakavyo elekezwa na idara ya afya.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa tawi hilo Sayyid Muhandi Almayaliy, amesema: “Kuna mambo yaliyokua yanafanywa na tawi hili, mengi yalisimama kutokana na janga la virusi vya Korona na baadhi yakaanza kufanywa kwa kutumia mitandao ya kijamii, baada ya kuanza kurudi hali ya kawaida kidogo kidogo tumepanga kuanza kutoa mhadhara wa tafsiri ya Quráni kila wiki”.

Akaongeza kuwa: “Tunamshukuru Mwenyezi Mungu, tumefika mhadhara wa tatu uliotolewa na Shekh Ali Aqili mmoja wa walimu wa hauza, amezungumzia aya tukufu ya (102) katika surat Swafaat isemayo (Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akajilaza juu ya jabali), akabainisha kuwa Ibrahim (a.s) alitambua ndoto yake ni amri ya kumchinja mwanae, hivyo akatafuta ushauri kutoka kwa mtoto wake na kuangalia atamjibu nini, akamjibu (Tenda unacho amrishwa) hakusema: nichinje. Anamaanisha kuwa baba yake ameamrishwa jambo ambalo lazima alifanye na kutii”.

Kumbuka kuwa mihadhara hii inatolewa chini ya mkakati maalum wa kulea jamii kupitia visa mbalimbali vya Quráni, na unalenga watu wa tabaka tofauti katika jamii ya wakazi wa Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: