Kamati ya afya imetembelea shule ya Sayyidu Al-Maa na kuangalia utekelezaji ya maelekezo ya idara ya afya

Maoni katika picha
Jopo la watumishi wa idara ya afya ya mkoa wa Karbala limetembelea shule ya msingi ya wavulana Sayyidu Al-Maa ambayo ipo chini ya shule za Al-Ameed katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kuja kuangalia utekelezaji wa maagizo ya idara ya afya, na kuangalia namna ya kushirikiana kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa wanafunzi na walimu katika mazingira ya maambukizi ya virusi vya Korona, ziara hii ni sehemu ya ratiba iliyo andaliwa na idara ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, kwa ajili ya kuangalia mazingira ya kujikinga na maambukizi.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Ahmadi Kaábi, amesema: “Vitengo vyote vya shule za Al-Ameed vimechukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, vimelipa umuhimu mkubwa jambo hilo na vimeweka mpango mkakati wa swala hilo, hii ni moja ya ziara nyingi watakazo fanya kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa wanafunzi na walimu wao”.

Akabainisha kuwa: “Jopo la watumishi waliokuja kufanya ziara wamechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi, pamoja na kufuata utaratibu unaotumika ndani ya shule ulio wekwa na kamati ya afya, aidha wamekagua vifaa vilivyo andaliwa na kamati ya shume kwa ajili ya kuzuwia maambukizi kwa wanafunzi, ili kuweka salama mazingira ya usomaji na malezi”.

Baada ya ziara hiyo wageni wametoa pongezi kwa uongozi wa shule, kwa kuwajali walimu na wanafunzi wao, na kuthamini afya zao, kwa kufanya juhudi kubwa ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: