Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimeanza kazi kubwa ya uratibu tangu kuanzishwa kwake

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimeanza kazi ya kupangilia mawakibu zote zilizo chini yake katika mikoa ya Iraq, huu ndio uratibu mkubwa kufanyika tangu kuanzishwa kwake, ili kuweka utaratibu mzuri wa kiutendaji unao endana na kazi wanazo fanya, na kurahisisha utowaji wa huduma wakati wa maombolezo ya Husseiniyya ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Tumeongea na rais wa kitengo bwana Riyadh Ni’mah Salmaan kuhusu swala hilo, amesema kuwa: “Baada ya kukutana na viongozi wa mawakibu na wawakilishi kutoka mikoani, tumekubaliana kuweka utaratibu mzuri wa utendaji wetu, chini ya maelekezo tuliyotoa, hatua ya kwanza ya mfumo mpya ni kutoa vitambulisho vipya vinavyo tofautiana na vile vya zamani, mawakibu zote za kutoa huduma pamoja na za kuomboleza zilizopo kwenye orodha yetu zitapewa vitambulisho hivyo”.

Akaongeza kuwa: “Tumeandaa mpango kazi wa shughuli hiyo katika kila mkoa, mawakibu zitawasiliana na wawakilishi wa kitengo kwenye kila mkoa na kukabidhi nyaraka husika kwa ajili ya kutengenezewa vitambulisho, tumeanza na mkoa wa Bagdad na tutaendelea na mikoa mingine”.

Akasisitiza kuwa: “Kitambulisho kipya hakiwezi kufojiwa, kimetengenezwa kisasa zaidi jambo ambolo haitawezekana kukichakachua au kutoa feki yake, pia kina namba maalum za siri, sambamba na wasifu wa mwenye kitambulisho, kitatumika kwa muta wa miaka mitano, baada ya muda kuisha kitarudishwa kwa mamlaka husika, wakati vitambulisho vya zamani vikiua vinatolewa kila mwaka na vilikua vinawahi kuharibika”.

Kumbuka kuwa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kinawajibika kuratibu utendaji wa mawakibu zoto, pamoja na kutoa vitambulisho na kuwatambua viongozi wa mawakibu kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi za kijamii na kiraia zinazo saidia mawakibu na vikundi vya Husseiniyya ni wasaidizi tu, haziwajibiki kisheria kuratibu shughuli za mawakibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: