Toleo la muongozo wa mwanafunzi katika kusoma kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Kamati ya elimu katika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, imetoa muongozo wa mwanafunzi katika kusoma kwa njia ya mtandao ambao ni miongoni mwa matoleo ya chuo kwenye sekta ya kujifunza kwa njia ya mtandao, toleo hili linaendana na mazingira ya sasa ambayo taasisi za elimu zinapitia duniani kote pamoja na Iraq, kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, na kutumiwa mitandao kama moja ya njia kubwa za kufikisha masomo kwa wanawafunzi.

Tumeongea na mjumbe wa kamati ya elimu Dokta Dhiyaau Karim Abdu Ali kuhusu swala hilo amesema kuwa: “Hakika kamati ya elimu inayo ongozwa na rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali, imechukua jukumu la kufikisha masomo kwa wanafunzi kwa kutumia njia rahisi, toleo hili lenye kurasa (81) ni sehemu ya utekelezaji wa jukumu hilo, limejaa maelekezo ya namna ya kusoma kwa njia ya mtandao, na yamepasishwa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu kutokana na janga la taifa la uwepo wa maambukizi ya virusi vya Korona, na athari yake katika maisha ikiwa ni pamoja na kwenye sekta ya elimu”.

Akafafanua kuwa: “Lengo la toleo hili ni kwamba chuo cha Al-Ameed kinafanya kila aina ya njia kuhakikisha kinaendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wake kwa kutumia mitandao, katika mazingira haya magumu kimasomo, na kutoa furasa kwa wanafunzi ya kupata masomo yote kwa njia ya mtandao na kuwawezesha kubadilishana elimu kwa njia hiyo, na kuwafanya waendane na teknolojia za kisasa sambamba na kushiriki kwenye majukwaa ya kielimu, yatakayo wawezesha kunufaika na masomo wanayo pata wakati wowote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: