Kuanza kazi ya ujenzi wa mradi wa jengo la Quráni

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameanza kujenga kituo cha Quráni kitakacho kua chini ya Maahadi ya Quráni tukufu, ili kuweza kukidhi upanuzi wa miradi ya Quráni inayo fanywa na Maahadi, na kuandaa sehemu maalum inayo endana na miradi hiyo ili kuendelea kufundisha utamaduni wa Quráni, imechaguliwa sehemu katika jengo la Alqami lililopo barabara ya (Baabil – Karbala) yenye ukubwa wa mita za mraba (1300).

Mhandisi Muhammad Mustwafa Twawiil kiongozi wa idara ya ujenzi katika kitengo tajwa amesema kuwa: “Tunajenga mradi huu kufuatia mahitaji ya Maahadi, jengo litakua na kumbi za madarasa (11) yatakayo tumika kufundishia na kufanya warsha za Quráni, huku vyumba (20) vitakavyo tumika kukaa wanafunzi, pamoja na uwezekano wa kuvitumia wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu kwa kulala mazuwaru na watumishi, hali kadhalika kuna chumba cha ofisi na ukumbi wa mikutano wenye ukubwa wa mita za mraba (250), pia kuna studio na sehemu ya vyoo”.

Akaongeza kuwa: “Ujenzi unaendelea kama ulivyo pangwa, ulikua umesimama kwa sababu ya kushughulishwa na ujenzi wa vituo vya Alhayaat, Insha-Allah kitakamilika ndani ya muda uliopangwa, kikiwa katika ubora mkubwa unao endana na malengo ya kujengwa kwake, na kitawekwa mitambo ya kisasa zaidi itakayo kifanya kuwa kituo cha mfano”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu imekuwa ikipanua utendaji katika miradi yake jambo ambalo limelazimika kuongeza jengo, harakati zake za miradi ya Quráni hufanyika katika kipindi chote cha mwaka, hufanya semina, warsha, nadwa na makongamano ambapo hualika watu tofauti katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: