Kuratibu semina ya watumishi wa kulinda nidham

Maoni katika picha
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa semina ya watumishi wa kitengo cha kulinda amani, ambayo ipo katika orodha ya semina za kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo hicho.

Dokta Muhammad Hassan Jabiri rais wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu amesema kuwa: “Hakika kitengo chetu kinaendelea kutekeleza wajibu wake kwa kutoa semina mbalimbali kwa watumishi, chini ya utaratibu wa kuwajengea uwezo watumishi wa vitengo vya Ataba tukufu, hii ni miongoni mwa semina muhimu inayo lenga kuboresha utendaji wa watumishi”.

Akaongeza kuwa: “Mada tofauti zimetolewa katika semina hii, miongoni mwa mada hizo ni:

  • - Mafundisho ya Akhlaq na Aqida.
  • - Mawasiliano na mbinu za kusimamia ofisi.
  • - Uwajibikaji kazini.
  • - Kujenga kujiamini”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunatarajia baada ya semina hii washiriki wawe na uwelewa zaidi wa mambo ya dini na wapambike kwa tabia za Ahlulbait (a.s), sambamba na kutumia njia nzuri za kuwasiliana na watu wengine pamoja na watumishi wenzao, sambamba na kuongeza ufanisi kwa ujumla katika utekelezaji wa majukumu yao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: