Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki kwenye hafla ya siku ya ushindi katika chuo kikuu cha Baabil

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia ugeni wa Multaqal-Qamaru chini ya kitengo cha habari na utamaduni, imeshiriki kwenye hafla iliyo andaliwa na chuo kikuu cha Baabil ya kuadhimisha tangazo la siku ya ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh.

Hafla imehudhuriwa na viongozi wa makundi tofauti pamoja na askari, bila kusahau walimu kutoka vyuo mbalimbali na wakuu wa vitivo na wanafunzi, wakitanguliwa na rais wa chuo Dokta Qahtwani Hadi Jaburi.

Atabatu Abbasiyya ilipata nafasi ya kuongea katika hafla hiyo, ikawakilishwa na Ustadh Hassan Jawadi kutoka kituo cha Alqamar, akasema: “Tunajivunia kumbukumbu hii na tunaichukulia kuwa siku muhimu sana kwa raia wa Iraq, kuikumbuka kunamaanisha kukumbuka uzalendo wa wairaq na namna walivyo pigania taifa hili na maeneo matakatifu, wakajitolea roho zao kwa ajili ya kuzuwia isichafuliwe na magaini wa Daesh, ushindi uliopatikana yalikua ni matokeo ya kusimama pamoja na Marjaa Dini mkuu na kufanyia kazi fatwa yake ya jihadi kifaya, kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu tulifanikiwa kuharibu njama za magaidi na kuwatoa katika maeneo waliyokua wameteka”.

Akaeleza pia nafasi kubwa ya vijana wa Iraq katika vita hiyo, akawaomba wasikilizaji wachukue mazingatio kwa vijana hao namna walivyo shikamana na kupigania taifa lao hadi wakapata ushindi, hususan mashahidi ambao ni kielelezo kikubwa cha kujitolea kwa ajili ya taifa.

Katika hafla hiyo mayatima thelathini kutoka familia za mashahidi wakapewa zawadi, na kulikuwa na ratiba ya soko la wahisani kwa mayatima, pamoja na maonyesho ya picha za mashahidi chini ya usimamizi wa kamati ya Hashdu-Shaábi, na ikakaribishwa familia ya shahidi Ahmadi Muhanna Laami.

Rais wa chuo akatoa shukrani nyingi kwa idara ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuhudhuria kwenye hafla hii na kushiriki kwenye ratiba yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: