Uwekaji wa miamvuli (34) inayosogea katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu

Maoni katika picha
Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya kiwefunga miavuli (34) inayosogea kwenye eneo linayo zunguka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi kwenye malalo ya ndugu yake Imamu Hussein (a.s), pembezoni mwa uwanja huo, ili kuwalinda mazuwaru na jua.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, ulikua na idadi kadhaa ya miamvuli hii, lakini kutokana na mazingira ya sasa tumeamua kuongeza miavuli hii baada ya kutengenezwa na mafundi wa Ataba tukufu, miamvuli hiyo ina mataili nguzo na paa, ipo (34) na imewekwa pande mbili za uwanja kwa mpangilia mzuri, usio tatiza matembezi ya mazuwaru wala kuharibu muonekano wa uwanja, itasaidia kutoa kivuli kwa mazuwaru hususa wanafamilia”.

Akaongeza: “Miamvuli hii inasogezeka kwa urahisi kutoka sehemu moja hadi nyingine, tayali wameshapangwa watumishi maalum watakao simamia kazi hiyo, paa la mwamvuli limetengenezwa kwa kitambaa chenye uwezo wa kuvumilia jua na kupambana na mazingira ya hewa, kila mwamvuli unaukubwa wa (mt 6 x 6) na urefu wa (mt 3.5)”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya siku za nyumba ilitengeneza karibu miamvuli (200) kwa ajili ya kutumiwa na mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ili kuwalinda na jua pamoja na mvua, ikasambazwa sehemu mbalimbali zinazo zunguka haram tukufu na kwenye viwanja vilivyo karibu na haram.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: