Kuanza kazi ya ukarabati na ujenzi wa mlango wa pili kwa ukubwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kukarabati na kujenga mlango wa Imamu Hassan (a.s), uliopo upande wa kusini magharibi ya haram tukufu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambao ni mlango wa pili kwa ukubwa baada ya mlango wa Kibla, unaangalia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kazi hii ni sehemu ya mradi wa kukarabati milango ya malalo takatifu, milango hiyo inatengenezwa kwa uhodari na umaridadi mkubwa, hatua ya kwanza ilihusisha mlango wa Imamu Haadi (a.s) uliopo upande wa kaskazini mashariki ya haram tukufu, na mlango wa Imamu Alkaadhim (a.s) uliopo mashariki magharibi ya haram.

Rais wa kitengo hicho Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaighi ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu kazi hiyo, amesema kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu inaipa umuhimu mkubwa milango yote ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ukizingatia kuwa imefungamana na mradi mkubwa wa upanuzi wa Ataba takatifu, milango hiyo ni sehemu ya muonekano wa jengo hilo na inatengenezwa kwa umahiri na ubora mkubwa”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya ukarabati na ujenzi wa milango hiyo itaunganishwa na milango ya zamani chini ya ufundi wa zamani na wa kisasa, na kuifanya kuwa na muonekano mzuri zaidi, kazi ya ukarabati wa mlango wa Imamu Hassan (a.s) ni sehemu ya mradi huo, nao ni mlango wa pili kwa ukubwa baada ya mlango wa Kibla, huchukuliwa kuwa mlango mkuu wa kuingilia mawakibu na mazuwaru wakati wa msimu wa ziara”.

Akafafanua kuwa: “Hatua ya kwanza imehusisha uondoaji wa vifaa vya ujenzi vya zamani, na kukarabati kuta zake pamoja na kuweka baadhi ya mifumo inayo hitajika, kazi zote zinafanywa bila kuufunga kutokana na umuhimu wake, kwa hiyo kazi imepangwa sehemu mbili ili kurahisisha harakati za mazuwaru”.

Akamaliza kwa kusema: “Mafundi wa shirika linalo tekeleza mradi huo, wameandaa ratiba ya ukarabati wa milango yote, mmoja baada ya mwingine kwa namna ambayo itaendana na ubora wa jengo kwa nje na ndani ya haram tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: