Atabatu Abbasiyya inasaidia katika ukarabati wa mazaru ya Sayyid Ali bun Hamza

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia watumishi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi, inasaidia ukarabati wa mazaru ya Sayyid Ali bun Hamza (r.a), kwa kutoa gari linalo saidia kuhudumia mazuwaru wa mazaru hiyo na wale wanao kwenda kuzuru malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwani ipo katika moja ya njia muhimu zinazo elekea kwenye Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, nayo ni moja ya mazaru mashuhuri na kituo cha kupumzika mazuwaru hasa wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Msimamizi wa kazi hiyo na kiongozi wa idara ya majengo na kitengo tajwa, Mhandisi Muhammad Mustwafa Twawiil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mradi huu ni sehemu ya miradi inayo saidiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwenye taasisi za kutoa huduma na mazaru zilizopo ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala, ni miongoni mwa kazi zinazo saidia kuboresha huduma kwa mazuwaru”.

Akaongeza kuwa: “Kazi walizopewa watumishi wetu na Ambazo tunafanya baada ya kukubaliwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya zimehusisha sehemu muhimu ambayo ni ujenzi wa vyoo katika mradi wa upanuzi wa mazaru hiyo, tunajenga vyoo (42) katika jengo la ghorofa mbili, vyoo vya wanaume na wanawake, vyenye kila kitu kinacho hitajika kwenye vyoo vya kisasa”.

Akasisitiza kuwa: “Kazi inaenda kama ilivyo pangwa tayali tumemaliza kuskimu ukuta katika ghorofa ya kwanza na kazi inaendelea ya kuweka marumaru za ukutani, na kwenye ghorofa ya pili tunaendelea na kukata vyumba vya vyoo na vyumba vya ofisi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: