Ratiba ya asubuhi (ya kuzaliwa jua la Zainabiyya) inayo fanywa na Maahadi ya Quráni tawi la wanawake, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kuadhimisha kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s) katika asubuhi ya mashairi iliyo fanywa kwa njia ya mtandao wa (ZOOM) asubuhi ya leo mwezi (3 Jamadal-Uula 1442h) sawa na tarehe (29 Desemba 2020m), wameshiriki washairi kutoka ndani na nje ya Iraq.
Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi amesema kuwa: “Usomaji wa mashairi utafanyika wiki nzima na kutakua na mambo mengine yanayo husu kuadhimisha kuzaliwa kwake na kuzungumzia utukufu wake, ikiwa ni pamoja na kueleza uaminifu wake, subira yake na msimamo wake pamoja na mazingira magumu aliyo pitia, na kutoa wito wa kupambika kwa tabia zake na kunufaika na nuru yake ingáayo, inayo tokana na nuru ya babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu na baba yake Ali na mama yake Zaharaa (a.s)”.
Jaburi amesema kuwa: “Asubuhi ya mashairi imefunguliwa chini ya kauli mbiu isemayo (kwa jabali wa subira yameandikwa mashairi) ameshiriki pia mshairi Imani Da’bal kutoka Baharain, na Asmahani Aalu-Turaab kutoka Saudia – Qatiif, na Sukaina Audah kutoka Lebanon, na Rina Khawiladi kutoka Iraq – Najafu Ashrafu, na Ahuda Abdulwahidi kutoka Iraq – Bagdad, beti za mashairi yao zimezungumzia utukufu wa bibi Zainabu (a.s), na wakaimba kaswida zilizo amsha hisia za mapenzi kwa bibi huyo mtakatifu”.
Kiongozi wa idara ya habari katika Maahadi ya Quráni tawi la wanawake, Dokta Israa Akraqi amesema kuwa: “Hakika ratiba hii nzuri ya washairi kwenye maadhimisho haya, inatoa wito kwa waandishi wajitokeze kuandika utukufu wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) hususan bibi Zainabu (a.s), kuwasifu wao ni sawa na kusifu misingi ya utukufu uliojaa kwao, jambo hili ni muhimu sana katika wiki ya (kuzaliwa jua la Zainabiyya) kama hafla hii ilivyo andaliwa na Maahadi katika maadhimisho haya”.