Kuamza kwa shindano la kielimu la wanawake kuhusu uhai wa bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendesha shindano la wanawake lenye anuani isemayo (Sikuona ispokua mazuri), kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) bibi Hauraa Zainabu (a.s) na kuadhimisha kumbukumbu hiyo tukufu inayo sadifu siku ya Jumatatu mwezi tano Jamadal-Uula.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo hicho bibi Asmahani Ibrahim: “Shindano hili ni sehemu ya harakati za kituo cha utamaduni, pia ni sehemu ya kuangazia historia ya mama huyu mtakatifu, na kusaidia kumtambulisha kwa njia ya maswali kuhusu bibi Hauraa (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Shindano lilianza siku ya mwezi (3 Jamadal-Uula) na litaendelea hadi mwezi tano, kila siku kutakua na maswali mawili, baada ya kumaliza muda wa shindano ambao huendelea hadi saa kumi na mbili jioni kila siku hufanya uchambuzi wa majibu sahihi, kisha huyapigia kura majibu hayo na kutoa zawadi kwa waliofaulu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: