Hivi karibuni kituo cha turathi za Basra kimetoa kitabu cha (Ahmadi bun Issa bun Zaidi Almukhtafi)

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa kitabu cha (Ahmadi bun Issa bun Zaidi Almukhtafi na mitazamo yake katika Fiqhi na Aqida kwenye kitabu cha Amaali – masomo ya mkarana).

Makamo wa mkuu wa kituo Shekh Yasin Yusufu amesema kuwa: “Mlango wa kwanza imeandikwa historia ya maisha yake, sehemu ya kwanza inamaelezo ya maisha yake binafsi na sehemu ya pili historia yake kielimu na nafasi yake kisiasa, sehemu ya tatu imeandika watafiti wa zama zake na mazingira ya kisiasa, kijamii na kielimu, na kufafanua nafasi yake katika kila mazingira”.

Akaongeza kuwa: “Mlango wa pili umeandika maoni yake katika somo ya fiqhi na aqida yaliyopo kwenye kitabu cha (Amaali), kwa kuyagawa sehemu tatu: sehemu ya kwanza inaelezea kitabu cha Amaali, sehemu ya pili mitazamo ya kifiqhi katika mlango wa Ibadaat na Muamalaat, kuna mada tofauti zinazo saidia kuelewa kwa urahisi, sehemu ya tatu imeandika maoni ya Aqida pamoja na kulinganisha na maoni ya wanachuoni wengine”.

Akafafanua kuwa: “Kutokana na elimu iliyopo kwenye kitabu hicho, inakifanya kuwa kitabu muhimu katika maktaba za kiislamu, hususan za hapa Basra”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: