Mazingira ya shangwe na furaha yametanda katika kuta na korido za malalo ya kaka yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, hii ni kumbukumbu ambayo ulimwengu mzima umejaa furaha, kuzaliwa kwake kulileta nuru aridhini na mbinguni, kwa nini isiwe hivyo wakati yeye ni mtoto mwema wa Ali na Zaharaa na ndugu wa Hassanaini -Hassan na Hussein- (a.s).
Kuta za Ataba tukufu na korodo zake zimewekwa mapambo, na kuwekwa mabango yaliyo andikwa maneno mazuri ya pongezi, na kuwashwa taa za rangi ambazo huwashwa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika matukio ya furaha, sambamba na kuweka mauwa kwenye milango ya haram tukufu, na kupokea wageni wengi wanaokuja katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kumpa pongezi kwa tukio hili tukufu kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), mwaka huu wageni wengi wanakuja kuomba dua ya kuisha kwa balaa la virusi vya Korona, na nchi za waislamu zipate amani na utulivu.
Pamoja na hivyo Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba kamili kuhusu tukio hili, inayo endana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa, na yenye vipengele vingi.