Kugawa zawadi kwa mahafidhwaat wa Quráni tukufu

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imewapa zawadi wanafunzi walio shiriki kwenye semina ya (Lu-u lu-u maknuun) ya kuhifadhi kwa haraka, ambao wameweza kuhifadhi juzuu (23) za Quráni tukufu ndani ya muda mfupi usio zidi miezi tisa.

Kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi amesema kuwa: “Hakika ugawaji wa zawadi ni sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s), na sehemu ya ratiba ya wiki ya (kuzaliwa kwa nuru ya Zainabiyya) inayo ratibiwa na Maahadi katika kuhuisha kumbukumbu hiyo, zawadi hizi ni ishara ya kupongeza juhudi zao na kuwapa moyo wa kukamilisha juzuu zilizo baki ndani ya muda mfupi, pia ni kivutio kikubwa kwa marafiki zao ili watamani kujiunga nao, wanafunzi wameonyesha juhudi kubwa ya kuhifadhi Quráni katika mazingira haya ya janga la Korona tunayo ishi, kwao sio kikwazo cha kuzuwia kuendelea na kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu, walikua wanahifadhi juzuu zima ndani ya wiki mbili kwa kweli hili ni jambo kubwa wanastaki pongezi pamoja na wasimamizi wao”.

Akaongeza kuwa: “Kuwapa zawadi wanafunzi hawa watukufu ni sehemu ya huduma inayo tolewa na Maahadi kwa wanafunzi wa Quráni, ili kutoa ushawishi kwa wanafunzi wengine kujiunga na somo hilo, tutaendelea kusaidia kila mwanafunzi wa Quráni hususan wasichana, jambo ambalo linasaidia kufundisha utamaduni wa kusoma Quráni kwa wasichana”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: