Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na naibu wake Mhandisi Abbasi Mussawi wametembelea mradi wa Firdausi na mradi wa Awali ambayo ni miradi mikubwa ya kilimo na ya kimkakati inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, miradi hiyo inanafasi kubwa katika sekta ya kilimo hapa nchini, aidha ni katika mkakati wa kubadilisha jangwa la Karbala kuwa kijani kibichi na kurudisha sifa ya kilimo hapa nchini.
Katibu mkuu amefuatana na rais wa kitengo cha kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu na mkuu wa hospitali ya Alkafeel pamoja na mkuu wa miradi hiyo miwili ya kilimo, aliyekuwa anaeleza hatua za kilimo hicho na mavuno yanayo tarajiwa, aidha ametembelea vituo vya kuzalisha umeme wa jua na kusikiliza maelezo kuhusu umeme huo na namba unavyo fanya kazi katika mashamba hayo.
Mwishoni mwa ziara hiyo katibu mkuu amesifu kazi nzuri inayo fanywa kwenye miradi hiyo na kuwataka waendelee kukamilisha hatua zinazo fuata.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inamiradi mingi, inafanya kazi kubwa kwenye mradi wa kilimo katika mkoa wa Karbala na mikoa mingine, miradi hiyo inamchango wa moja kwa moja wa kusaidia upatikanaji wa chakula katika taifa.