Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwake: Kazi ya kutengeneza vipande vya dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) imeanza

Maoni katika picha
Sayyid Naadhim Ghurabi rais wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitakatifu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu amesema kuwa, tumeanza kutengeneza vipande vya dirisha jipya la bibi Zainabu (a.s), baada ya kupasishwa mchoro wake, kazi hii imeanza katika siku hizi za kuadhimisha kuzaliwa kwa yule ambaye dirisha hilo litawekwa juu ya kaburi lake takatifu bibi Hauraa (a.s).

Akaongeza kusema: “Miongoni mwa vipande vinavyo tengenezwa ni vile vinavyowekwa madini (sehemu inayounganisha kati ya eneo moja na lingine), sehemu imara (Stainless Steel) inayo tengenezwa kwa madini yasiyoshika kutu, vipande hivyo vipo (14), na tumeanza kutengeneza sehemu nyingine kwa madini ya fedha”.

Akabainisha kuwa: “Sehemu inayotiwa madini inaujazo wa (ml 3) na sehemu za kushika zinaujazo wa (ml 6), kila kipande kinatengenezwa kwa hatua mbili, hatua ya kwanza tunaweka madini na hatua ya pili inasawazishwa na ya kwanza na kinakua kitu kimoja”.

Akasisitiza kuwa: “Mafundi wanafanya kazi hiyo kwa bidii kubwa, ili waikamilishe ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora mkubwa, kazi zote zinaendelea vizuri siku chache zijazo tutakamilisha hatua hii na kuingia hatua nyingine”.

Akamaliza kwa kusema: “Kazi ya kutengeneza boma la mbao inaendelea na imeshapiga hatua kubwa, na litakamilika na kuwa tayali kuunganishwa na kipande chochote kilicho tengenezwa kwa madini”.

Kumbuka kuwa dirisha linatengenezwa na raia wa Iraq miongoni mwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na linatarajiwa kuwa na ubora mkubwa, mambo mengi yamezingatiwa yatakayo lifanya kuwa zuri na kuendana na paa lake lililo tengeneza siku za nyuma, pia linafanana na dirisha la zamani lililopo hivi sasa, bila kusahau kufanana kwake na dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: