Dokta Aamir Salim Amiir rais wa ugeni uliotoka wizarani na mmoja wa wajumbe wa idara ya utafiti na maendeleo katika wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu amesema kuwa, chuo kikuu cha Alkafeel ni moja ya taasisi ya elimu ya juu yenye maendeleo makubwa, kimekuwa mstari wa mbele daima katika usomeshaji wa njia ya mitandao.
Ameyasema hayo alipotembelea chuo hicho akiwa na jopo la wataalam kutoka wizarani, na kupokelewa na rais wa chuo Dokta Nuris Dahani na Dokta Farasi pamoja na Dokta Nawaal Almayali na wakuu wa vitivo, wageni wameangalia sehemu mbalimbali za chuo pamoja na vifaa vya kufundishia.
Akaongeza kuwa: “Hakika chuo kikuu cha Alkafeel kimekua mstari wa mbele na kinafanya vizuri daima katika levo ya vyuo binafsi, kwa sababu tunakifuatilia wakati wote, leo tumekuja kukitembelea na tumeona tofauti kubwa ya kile tulicho soma kwenye karatasi na mazingira halisi, kinaviwango vya kimataifa katika kila sekta, na kwa namna ya pekee chuo hiki kimepiga hatua kubwa katika sekta ya teknolojia za ufundishaji”.
Naye Dokta Uswaam Khalidi akasema kuwa: “Hakika chuo kikuu cha Alkafeel kutokana na tuliyo yaona, kipo makini sana kinaviwango vya kimataifa katika kila kitu, kuanzia majengo yake, kumbi za madarasa, maabara sambamba na kutimiza mkakati wa kimataifa wa maendeleo endelevu, bila kusahau vifaa vya kisasa wanavyo miliki”.