Jirani na malalo ya kaka yake: imefanywa hafla ya wanawake ya kukumbuka kuzaliwa kwa Swidiqatu-Sughura Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya hafla kubwa, ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa jemedari wa Karbala Aqilatu bani Hashim Zainabu bint Ali (a.s), ndani ya sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) katika Ataba tukufu, kwa kufuata kanuni zote za kujikinga na virusi vya Korona, kundi kubwa la mazuwaru na watumishi wamehudhuria kwenye hafla hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya bibi Taghrid Tamimi makamo kiongozi wa idara ya wahadhiri, amesema: “Hafla hii ni sehemu ya harakati za idara za kuhuisha na kuadhimisha tarehe za kuzaliwa kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na watu wanao fungamana nao, kila mwaka huwa tunafanya hafla hii, ili kueleza japo kwa kifupi historia ya bibi huyu mtakatifu, hafla imefunguliwa kwa Quráni tukufu halafu ukafuata ujumbe kuhusu umuhimu wa kufuata mwenendo wa jemedari wa Karbala, na kumfanya kuwa kielelezo cha mwanamke bora wa kuigwa, kama ulivyo zungumzwa uhai wake katika nyumba iliyotiwa nuru na Mwenyezi Mungu mtukufu, nayo ni nyumba ya Ali na Fatuma (a.s), nuru ambayo ilimfanya kuwa jemedari aliye onyesha msimamo imara pembeni ya kaka yake Imamu Hussein (a.s) katika vita ya Twafu”.

Akaongeza kuwa: “Hafla imepambwa na uimbaji wa kaswida za kumsifu Aqilatu-Hashimiyya (a.s) na tukio hili tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: