Kuanza usajili wa semina za Quráni kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Quráni katika Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, kimeanza kusajili wanafunzi watakaoshiriki kwenye semina za Quráni zitakazo endeshwa kwa njia ya mtandao kwa wanaume peke yake kutoka kila sehemu ya dunia, semina hizo ni sehemu ya mkakati wa kufundisha utamaduni wa kushikamana na Quráni na kutengeneza kizazi kinacho fanyia kazi mafundisho ya Quráni, kizazi chenye maadili mema yanayo tokana na mafundisho ya Quráni tukufu.

Kituo kimesema kuwa masharti ya kujiunga ni:

  • - Muombaji awe na umri wa miaka (18) na zaidi kwa semina zote za Quráni, ispokua semina ya maarifa ya Quráni, watakao kubaliwa kwenye semina hiyo ni wale wenye miata (20) na zaidi.
  • - Muombaji awe anakipaji cha sauti kama anataka kujiunga na semina ya fani za usomaji.
  • - Ajaze fomu kwa njia ya mtandao iliyo ambatana na tangazo, tambua kuwa mwisho wa kupokea fomu za kujiunga ni tarehe (25 Desemba 2020m).
  • - Kukubaliwa kutategemea matokea ya mtihani wa majaribio utakao fanywa kwa kutuma video isiyozidi dakika mbili (atakayo rekodi fani na adabu za usomaji), na kutumwa pamoja na fomu kwa njia ya mtandao.
  • - Tambua kuwa semina zitaanza tarehe (1 Januari 2021m) na linki ya kujiunga na semina hizo ni: https://docs.google.com/.../1FAIpQLScI..wform
    kwa maelezo zaidi piga simu namba (07602343344) kupitia whatsap au telegram.

Kituo kimetaja semina zitakazo tolewa ni:

  • - Semina ya maarifa ya Quráni.
  • - Semina ya hukumu za Quráni.
  • - Semina ya adabu za usomaji (sauti na naghma).

Kumbuka kuwa lengo la mradi huu ni:

Kwanza: Kuwapa nafasi watu wenye kipaji cha usomaji wa Quráni.

Pili: Kutengeneza kizazi cha wasomaji wa Quráni wenye elimu bora.

Tatu: Kusimama pamoja na maeneo muhimu katika turathi zetu kwenye sekta ya maarifa ya Quráni, kuhusu hukumu za usomaji tunafuata mapokezi salama na misingi sahihi, na fani za usomaji tumejikita katika ufuatiliaji wa kielimu na mafunzo endelevu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: