Kitabu cha (Tambihi ya maajabu ya Man-laa yahdhuruhu faqiihu) toleo jipya la kituo cha turathi za Basra

Maoni katika picha
Hivi kiribuni kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa kitabu cha (Tambihi ya maajabu ya Man-laa yahdhuruhu faqiihu) kilicho andikwa na Shekh Muflihu bun Hassan Saimariy Albaswariy Albaharaniy, ameandika kwa mfumo wake wa fiqhi mambo wa uwaziri katika ukurasa wa (234).

Makamo mkuu wa kituo cha turathi za Basra Shekh Yasini Yusufu akasema kuwa: “Hakika kitabu hiki asili yake ni nakala-kale zilizo patikana katika hazina ya kituo cha turathi, na kufanyiwa uhakiki kwa ajili ya kuziweka mbele ya wanafunzi na kuhuisha turathi za wanachuoni wa mji huu”.

Akaongeza kuwa: “Kitabu kimeandika mambo ya ajabu yaliyo tajwa na Shekh Swaduqu –r.a- katika kitabu chake cha (Man-laa yahdhuruhu faqiihu) na kubainisha baadhi ya mambo yenye ikhtilafu kwa wanachuoni mashuhuri wa umma miongoni mwa milango ya kifiqhi, pamoja na kujadili rai za wanachuoni katika jambo hilo kwa kuangalia hoja zilizo tolewa”.

Tambua kuwa kitabu hiki ni moja ya matoleo ya turathi ambayo kituo cha turathi za Basra kinacho jishughulisha na kuhuisha turathi za kiislamu na kuchangia kuingiza vitabu vya turathi katika maktaba sambamba na kuwapa wasomaji vitabu wanavyo weza kurejea katika masomo na tafiti zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: