Shule za Al-Ameed zinasherehekea kuzaliwa kwa bibi Zainabu Kubra (a.s)

Maoni katika picha
Shule za Al-Ameed zimefanya sherehe kubwa ya kuadhimisha kuzaliwa kwa bibi Zainabu Kubra (a.s), maadhimisho ya mwaka huu yamefanywa chini ya tahadhari kubwa ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na yalikuwa na vipengele tofauti vilivyo fanywa na wanafunzi.

Rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Ahmadi Kaábi amesema: “Kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa kwa bibi Zainabu Kubra (a.s), shule za Al-Ameed zimeadhimisha tukio hilo kwa kufanya hafla mbalimbali”.

Akabainisha kuwa: “Shule za Al-Ameed kupitia taasisi zake huadhimisha matukio ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) ikiwa ni pamoja na tarehe za kuzaliwa kwao na kufariki chini ya ratiba maalum ambayo hupangwa kila mwaka”.

Akaongeza kuwa: “Bila shaka maadhimisho haya hulenga kujaza mapenzi ya Ahlulbait (a.s) katika nafsi za vizazi na vizazi, sambamba na kufanyia kazi ujumbe usemao (Huisheni mambo yetu, Mwenyezi Mungu amrehemu atakaehuisha mambo yetu)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: