Kitengo cha Dini kinaangazia wahadhiri wa Karbala wa zama hizi

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinaangazia tabaka muhimu katika jamii nalo ni tabaka la wahadhiri, kupitia kitabu kiitwacho (wahadhiri wa Karbala wa zama hizi), juzu la kwanza la kitabu hicho limeandikwa wahadhiri wa mji huu mtukufu, wanao fikisha sauti ya Imamu Hussein ndani na nje ya mkoa huu mtukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya muandishi wa kitabu hicho Shekh Aamir Karbalai amesema: “Hakika toleo hili ni sehemu ya jibu la Dini kwa kundi hili muhimu katika kuhuisha maadhimisho ya Husseiniyya, tunamshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu, mji wa Karbala unawahadhiri wengi, kwa ajili ya kuwatambulisha kwa jamii tumeamua kuandika kitabu hiki, kitakuwa na juzuu nyingi na hili ndio juzuu la kwanza, ambalo tumeandika historia ya kila mhadhiri na kiwango chake cha elimu pamoja na uzuzi mwingine alio nao”.

Akabainisha kuwa: “Mhadhiri huchukuliwa kuwa mtu mwenye hazina nyingi, na yukotayali kutoa elimu yake kwa watu kulingana na uwezo wa akili zao, kutokana na kauli ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) isemayo: (Sisi mitume huongea na watu kulingana na uwezo wa akili zao), elimu ni amana ambayo hutakiwa kufikishwa kwa wahusika, kutoka kwa watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.

Akafafanua kuwa: “Kitabu kimeandika nasaha na maelekezo ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani aliyotowa kwa wahadhiri wa Husseiniyya”.

Tambua kuwa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, huandika vitabu kila baada ya muda fulani vinavyo husu dini, utamaduni na maelekezo mbalimbali, unakaribishwa kutembelea maonyesho ya vitabu ya kitengo cha Dini yaliyopo katika uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: