Zaidi ya dinari tirioni 8: zimetolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel kupitia huduma tofauti inazotoa bure

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imekua ikitoa huduma za matibabu bure zilizo igharimu zaidi ya dinari tirioni (8) ndani ya miaka mitano tu, bado hospitali inaendelea kutoa huduma bure kwa baadhi ya makundi ya wagonjwa, kama sehemu ya msaada wake wa kibinaadamu kwa wagonjwa hao.

Mkuu wa hospitali Dokta Jaasim Ibrahim amesema: “Wanufaika wa huduma hizo wametoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, ambao ni:

  • - Askari wa serikali na Hashdu-Shaábi bamoja na familia zao.
  • - Mafakiri na watu wenye kipato kidogo.
  • - Majeruhi wa maandamano ya islahi yaliyo fanyika mwaka 2019m.
  • - Wenye uwezo mdogo.
  • - Mayatima na familia zao.
  • - Makundi mengine walikua wanapewa punguzo la kiwango maalum”.

Akafafanua kuwa: “Huduma zilizo tolewa, imma zilikua zinatolewa ndani ya hospitali, kama vile upasuaji wa aina zote (mkubwa wa kati na mdogo), au nje kwa kutumia kikosi cha (matibabu bila malipo), hospitali ilitumia utaratibu wa kuwasiliana na muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu (Mu’tamadu-Marjaiyya) na mawakala wake au taasisi za kibinaadamu, au kwa mgonjwa kuja moja kwa muja hospitalini, pamoja na baadhi ya wagonjwa tulio wafikia kwa kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii”.

Naye kiongozi wa kitengo cha upasuaji katika hospitali hiyo Dokta Osama Abdulhassan amesema kuwa: “Hakika hospitali ilikua na mchango mkubwa katika miaka iliyopita, kwa kutibu askari waliojeruhiwa pamoja na wapiganaji wa Hashdu-Shaábi na makundi mengine, tumesaidia kuokoa majeruhi na wagonjwa waliokua katika hali mbaya sana, hali ambayo ilikua ni vigumu kutibiwa hapa Iraq, tuliwasaidia na kuacha kusafiri nje ya taifa, tumefanya upasuaji mbalimbali chini ya madaktari ambao ni raia wa Iraq pamoja na raia wa kigeni kutoka nchi za kiarabu na kiajemi, tumetumia teknolojia za kisasa zaidi”.

Akasisitiza kuwa: “Hakika hospitali inachumba cha upasuaji cha kisasa kilicho wasaidia madaktari kufanya upasuaji kwa mafanikio, chumba hicho kinafanya kazi kwa ubora wa kimataifa na kinatumia mfumo wa (I.S.O), kimesha fanya upasuaji mara nyingi kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa zaidi tofauti na upasuaji wa zamani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: