Kitivo cha uuguzi katika chuo kikuu cha Al-Ameed kinaendesha semina kwa wauguzi wa hospitali ya Alkafeel

Maoni katika picha
Kitivo cha uuguzi katika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kinaendesha semina kwa wauguzi wa hospitali ya rufaa Alkafeel, kama sehemu ya kuendeleza ushirikiano kwa faida ya pande mbili, na kubadilishana uzowefu kwa ajili ya kutoa huduma bora za uuguzi kwenye hospitali hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kitivo cha uuguzi Dokta Dhiyaau Karim Abayati, akaongeza kuwa: “Semina hii inatokana na ratiba ya huduma kwa jamii zinazo tolewa na chuo kikuu cha Al-Ameed kwa ujumla pamoja na kitivo cha uuguzi, chini ya ujumbe wa kielimu na kibinaadamu unaolenga kutuma watumishi mbalimbali, ikiwa pamoja na kufanya semina za aina tofauti, ikiwemo semina hii inayolenga wauguzi wa hospitali ya Alkafeel, daima hospitali imekuwa mstari wa mbele katika kuboresha uwezo wa watumishi wake, na tabaka la wauguzi ni miongoni mwa watumishi wake muhimu”.

Akabainisha kuwa: “Ratiba ya semina inasaa (150) za masomo, yamegawanywa sehemu mbili: kwanza ni masomo ya nadhariya, yanajumuisha utowaji wa mihadhara ya kielimu, na sehemu ya pili ni vitendo, navyo vinakamilisha sehemu ya kwanza kwa kufanyia kazi mambo yaliyo fundishwa kwa nadhariya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: