Kuanza kuandaa waraka wa maelezo ya wanachuoni wa Karbala na turathi zake

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia idara ya faharasi ya nakala kale kimeanza kuandaa waraka wa maelezo ya wanachuoni na turathi za mji mtukufu wa Karbala.

Mkuu wa kituo ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Hakika kituo kinafanya kazi ya kuhakikisha kinapata mafanikio mfululizo bila kukatika, kimegawa majukumu kwa ofisi zilizo chini yake, na kuweka mpango kazi kamili pamoja na makadiria ya muda (time frame) kwa kila mradi”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya kuweka mkakati na mpango kazi tumeanza kutekeleza, tumeanza kuandika waraka kuhusu wanachuoni wa Karbala na nafasi zao, na nakala-kale za watumishi wa haram, tumefanikiwa kukamilisha mahitaji ya jambo hilo na kuandaa mada tofauti, miongoni mwa mada hizo ni:

  • - Turathi zilizo chapishwa katika baadhi ya majarida, likiwemo jarida la (Mirathu hadithu-shia).
  • - Wanachuoni na vitabu vyao, tutabainisha vitabu vilivyo chapishwa na visivyo chapishwa, na upatikanaji wa nakala-kale na vitabu vilivyo chapishwa”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunafanya kazi kwa bidii kubwa ili tukamileshe kwa asilimia %100, waraka huu utasaidia kukipatia kituo taarifa za awali zinazo hitajika katika miradi ya uhakiki na uandishi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: