Hatua ya mwisho katika ujenzi wa jengo la ofisi za Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Mafundi wanaofanya kazi katika jengo la ofisi za Atabatu Abbasiyya tukufu wapo katika hatua ya mwisho, litaongeza sehemu za kuhudumia mazuwaru ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwani idadi kubwa ya vitengo vinavyo tumia haram hiyo kutoa huduma vitahamia kwenye jengo hilo.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huu ni mradi muhimu, unajengwa kisasa katika hali inayo endana na huduma zinazo tolewa na vitengo vya Ataba tukufu, kazi inayo endelea sasa hivi kwa asilimia kubwa ni umaliziaji, kwa ujumla kazi inaendelea vizuri kila sehemu na itakamilika ndani ya muda uliopangwa, hatua ijayo itakuwa ya kuweka vifaa vinavyo hitajika katika kila kitengo kulingana na kazi zao”.

Kumbuka kuwa mradi unajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa (2m1395) jengo linaghorofa kumi, eneo la tabaka ya chini linaukubwa wa mita (1100) litatumika kuegesha magari, sehemu ya chini itakua na ofisi za mapokezi, kuanzia ghorofa la kwanza hadi la nane kutakuwa na ofisi za vitengo vya Ataba, kila ghorofa linaukubwa wa (2m1250).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: