Kiongozi wa kiwanda Ustadh Farasi Ibrahimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu bidhaa wanazo tengeneza kwa kusema kuwa: “Kiwanda cha kutengeneza madaftari kinafanya mchakato wote kuanzia kutengeneza karatasi nyeupe kisha kupiga mistari, kukata, kutengeneza majarada, kukata na kuhesabu, tunatengeneza jumla ya daftari (100,000) kwa siku, madaftari hayo hukamilika katika kila kitu tena kwa ubora mkubwa, tunatengeneza daftari (502) kwa dakika hiyo ni kasi kubwa na kwa ubora wa hali ya juu, mitambo yetu inasifa zifuatazo:
- 1- Uwezo wa kuchapisha madaftari ya saizi zote na lugha tofauti (Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kihindi).
- 2- Karatasi bora zenye uzito mzuri na rafiki kwa mazingira.
- 3- Zinanguka kwa urahisi.
- 4- Rangi zake ni nzuri na haziumizi macho.
- 5- Zinamuonekano wa kuvutia chini ya ubunifu wa Daru.
- 6- Zinatengenezwa Iraq na sehemu ya uboreshaji wa viwanda vya Iraq.
- 7- Bei yake ni nafuu ambayo kila mtu anaweza kuimudu.
- 8- Bidhaa za ndani zinasaidia kukuza uchumi wa taifa na kulinda uchumi kwa kuacha kuagiza kutoka nje ya taifa.
- 9- Kuna aina mbili za majalada: mepesi na magumu”.
Akafafanua kuwa: “Hatujaishia kwenye kutengeneza madaftari peke yake, bali tunatengeneza pia karatasi za saizi zote (A4, A3, A5, A6) zenye mistari na zisizokuwa na mistari”.
Akasisitiza kuwa: “Hakika bidhaa zetu zinaweza kukidhi mahitaji ya wizara ya malezi na elimu ya Iraq kwa ukamilifu, kwa maelezo zaidi kuhusu uzalishaji wetu tembelea kiwanda kilichopo katika mkoa wa Karbala tukufu –Ibrahimi- sehemu ya Saqaa/2, karibu na chanel ya Karbala, au piga simu kwa namba zifuatazo: (07706733834/ 07823950890/ 07602335433) au tuandikie kwa barua pepe ifuatayo: dar-alkafeel@outlook.com.