Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanza kuweka vifaa kwenye jengo la afya, na kuweka kila kinacho hitajika kwa ajili ya kupokea wanafunzi katika mwaka mpya huu wa masomo.
Makamo rais wa chuo katika mambo ya taaluma Dokta Nawaal Almyali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika chuo kimesha kamilisha mahitaji yoto ya lazima, yanayo endana na mahitaji ya usomaji kama vile mbao za kisasa, viti vya wanafunzi maabara zenye vifaa vyote muhimu na vya kisasa vinavyo mfanya mwanafunzi ajihisi yupo kwenye chuo cha kimataifa sawa na vyuo vingine vikubwa duniani”.
Akasisitiza kuwa: “Mambo yaliyo kamilika ni msaada mubwa katika usomaji wa wanafunzi, na yametimiza vigezo na muongozo wa wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu chini ya mazingira ya janga la virusi vya Korona, vyumba vya madarasa na maabara vimewekwa vifaa vya kisasa zaidi”.
Kazi ya umaliziaji wa jengo zipo katika hatua ya mwisho, hayo yamesemwa na Mhandisi mkazi Ali Husaam, akaongeza kuwa: “Kazi inayo endelea hivi sasa ni kuweka marumaru ukuta wa mbele, kazi inafanywa kwa ubora mkubwa na kwa kufuata maelekezo ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, kiwanja kinaukubwa wa mita (1300) na jengo linaghorofa tano zenye jumla ya mita za mraba (6500), na jumla ya vyumba (12) vya madarasa, vyumba vitatu vinaukubwa wa mita (195) kila kimoja, na vyumba vitatu kila kimoja kina ukubwa wa mita (160), vingine vitatu vinamita (145) kila chumba, na vyumba vya maabara (12), vitatu katika hivyo kila kimoja kinaukubwa wa mita (150), huku vyumba vingine vikiwa na ukubwa tofauti, pia kuna vyumba vya ofisi na vyoo pamoja na ngazi za umeme”.
Kumbuka kuwa mradi huu unajengwa na shirika la Liwaau-Al-Aalamiyya chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, nao ni muendelezo wa majengo yaliyokamilika kama vile: “kitivo cha famasia, kitivo cha udaktari, kitivo cha uhandisi), pamoja na jengo la utawala.