Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kamati ya maelekezo na misaada, kimeratibu majlisi ya kuomboleza katika Husseiniyya ya Ahlulbait (a.s) wilaya ya Khaniqina mkoa wa Diyala, kwa ajili ya kuomboleza kifo cha pande la damu ya Mtume (s.a.w.w) bibi Fatuma Zaharaa (a.s), na imeendelea kwa muda wa siku tatu.
Kiongozi wa kamati tajwa aliyeshiriki katika uombolezaji huo Shekh Haidari Aaridhwi, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika kitengo hiki hufanya harakati ndani na nje ya mkoa mtakatifu wa Karbala katika kukumbuka siku za huzuni kwa Ahlulbait (a.s), miongoni mwa matukio hayo ni hili la kumbukumbu ya kifo cha bibi Zaharaa (a.s), tumefanya majlisi za kuomboleza kwenye husseiniyya kwa muda wa siku tatu na ilikuwa na vipengele vingi, ilikuwa inafunguliwa kwa Quráni tukufu kisha unafuata muhadhara wa kidini, ambapo mambo muhimu yamebainishwa ikiwa ni pamoja na majina ya sifa (laqabu) za bibi Zaharaa (a.s) pamoja na historia yake na nafasi kupwa aliyonayo mbele ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyo elezwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) katika hadithi nyingi, miongoni mwa hadithi hizo ni: (Yeye ni roho iliyo baina ya mbavu zangu) na (Fatuma ni pande la damu yangu), tumetoa wito wa kupambika kwa tabia nzuri alizokuwa nazo Zaharaa (a.s), pamoja na kueleza vipengele muhimu katika kulingania kwake uislamu”.
Majlisi zikahitimishwa kwa kueleza tukio la kifo chake (a.s), na matukio makubwa yaliyo fanyika hususan kushambuliwa kwa nyumba yake, pia tulijibu maswali ya wasikilizaji, mwisho wa kila mhadhara tuliinua mikono na kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu aharakishe faraja ya Aali Muhammad na awarehemu waumini wote, alilinde taifa la Iraq dhidi ya maadui na kuwarehemu mashahidi wetu na atuondolee hili janga.