Kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake wa duniani bibi Zaharaa Albatuli (a.s)

Maoni katika picha
Siku ya mwezi (13 Jamadal-Uula) ni kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake wa duniani na pande wa damu ya Mtume (s.a.w.w) na mke wa kiongozi wa waumini (a.s) na mama wa maimamu watakasifu (a.s), Fatuma Zaharaa mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa riwaya.

Imepokewa katika kitabu cha Kashful-Ghumma na vinginevyo kuwa: alipokaribia kufa alimuambia Asmaa bint Umais amletee maji, akatawadha na inasemekana alioga na akajipuliza marashi na akavaa nguo mpya kisha akamuambia Asmaa: Jiburili (a.s) alikuja kwa Mtume (s.a.w.w) alipokaribia kufa akiwa na Kafuur kutoka peponi, Mtume (s.a.w.w) akaigawa kafuur hiyo sehemu tatu, sehemu yake, ya Ali na yangu, ilikuwa dirham arubaini.

Akasema: Ewe Asmaa niletee marashi ya baba yangu yaliyo baki na uyaweke kichwani kwangu, kisha akajifunika nguo yake na akasema: Niache kidogo kisha unite nikiitika vizuri na nisipo itika ujue nimeshaenda kwa baba yangu.

Nikasubiri kidogo kisha nikamwita hakunijibu, tuliita; Ewe mtoto wa Muhammad ewe mtoto wa mbora wa wanawake, ewe mtoto wa mbora wa viumbe, ewe mtoto wa yule aliyekuwa karibu na Mola wake kwa umbali wa upinde au karibu zaidi ya hapo.

Akasema: hakujibu, nikafunua uso wake nikakuta tayali amesha kufa, nikambusu huki nikisema: Ewe Fatuma utakapoenda kwa baba yako Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) mpe salamu kutoka kwa Asmaa binti Umais.

Hassan na Hussein na mama yao (a.s):

Wakati akiwa amemkumbatia na kulia wakaingia Hassan na Hussein wakasema: Awe Asmaa kitugani kimemfanya mama alale katika muda huu? Akasema: Enyi watoto wa Mtume (s.a.w.w) mama yenu hajalala amefariki, Hassan akamkumbatia mama yake huku anasema: Ewe mama yangu niongeleshe kabla ya roho yako kuondoka kwenye muili, naye Hussein akawa anabusu miguu yake huku anasema: Ewe mama yangu mimi ni mwanao Hussein nizungumzishe kabla moyo wangu haujapasuka nikafa, Asmaa akawaambia: Enyi watoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu nendeni kwa baba yenu Ali mkamuambie kufariki kwa mama yenu, wakaenda hadi walipo fika karibu na msikiti sauti ya kulia kwao ikawa kubwa, maswahaba wakawafuata na kuwauliza nini tatizo, kitu gani kinawaliza enyi watoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, au mmemkumbuka babu yenu (s.a.w.w) ndio maana mnalia? Wakasema: hapana mama yetu Fatuma (a.s) amekufa, Ali akaanguka chini kwa uso wake huku akisema: majonzi yaliyoje ewe binti wa Muhammad? Nilikuwa najivunia wewe sasa nani tajivunia?

Akawa ameondoka Zaharaa (a.s) akiwa mwenye ham ya kukutana na Mola wake pamoja na baba yake, alifariki wakiwa na majeraha makubwa na uchungu mwingi, amekwenda kushtaki kwa Mwenyezi Mungu mtukufu ahukumu kati yake na wale waliomdhulumu haki yake, Imamu Ali (a.s) akasimama na akaenda kumuosha na kumvisha sanda kisha akaita: (ewe Hassan.. ewe Hussein.. ewe Zainabu na Ummu-Kulthum, ageni na kukutana ni peponi), baada ya muda mfupi akawatoa kwa mama yao (a.s).

Kisha Ali akaongoza swala ya jeneza na alipo maliza akainua mikono na kusema: (Ewe Mola huyu ni mtoto wa Mtume wako Fatuma, mtoe katika giza na kumtia kwenye nuru itakayo angaza maili na maili), Ali (a.s) akamuingiza kaburini na akamuweka kwenye mwanandani kisha akatoka, waliokuwepo wakafunika kaburi lile kwa udongo, halafu Ali (a.s) akalisawazisha na likawa halijulikani lilikuwa wapi na litaendelea kutojulikana hadi siku ya kiyama.

Amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa na siku aliyokufa akiwa ni mwenye kudhulumiwa na siku atakayo fufuliwa akiwa ni mwenye kuridhia na kuridhiwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: