Idara ya faharasi katika kituo cha turathi za Hilla imefanya kazi kubwa ya kutengeneza faharasi na kupangilia turathi za Hilla

Maoni katika picha
Idara ya faharasi katika kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni moja ya idara muhimu katika kuhuisha turathi za malikale na utamaduni wa mji wa Hilla, inafanya kazi kubwa ya kukusanya taarifa kuhusu turathi na kuzifanyia uhakiki.

Katika kuangazia kazi wanazo fanya tumeongea na mkuu wa kituo hicho Shekh Swadiq Khawilidi amesema kuwa: “Kazi ya kutengeneza faharasi inategemewa sana katika shughuli za uhakiki na utafiti kituoni, kutokana na umuhimu wake, kwani kuwepo kwa taarifa za faharasi husaidia kufanya tafiti na uhakiki na kuifanya kazi kwa ufanisi mkubwa”.

Akasisitiza kuwa: “Idara ya faharasi inakazi kubwa, ndio msingi wa sekta ya uhakiki na tafiti, husaidia kutafuta taarifa na kupata mambo yanayo hitajika kwa ajili ya uhakiki, ikiwa ni pamoja na picha za vitu hivyo, sambamba na kuweka taarifa za vitabu vinavyo andikwa na kituo hicho”.

Kumbuka kuwa idara ya faharasi katika kituo cha Hilla inafanya kazi kubwa ya kutafiti na kuhakiki turathi, ni tegemeo la waandishi na watafiti wa mambo yanayo husiana na turathi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: