Mkuu wa tarbiyya wa mkoa wa Karbala ametembelea shule ya Al-Ameed na Al-Qamaru

Maoni katika picha
Ustadh Abbasi Audah Sultani kiongozi mkuu wa tarbiyya katika mkoa mtukufu wa Karbala, ametembelea shule ya Al-Qamaru na Al-Amee ambazo zipo chini ya kitengo cha malezi na elimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu ikiwa ni sehemu ya ratiba yake ya kutembelea shule na kukagua ubora wa elimu.

Amekagua madarasa na kukutana na viongozi wa shule pamoja na kuangalia maendeleo ya wanafunzi na kazi inayofanywa na idara, ya kuheshimu na kutekeleza maelekezo ya wizara ya elimu na wizara ya afya, amesema kuwa yupo tayali kutoa ushirikiano wowote utakao hitajika.

Uongozi wa shule ya Al-Ameed na Al-Qamaru umesisitiza umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kutekeleza malengo ya kuanzishwa shule hizo, na kuzifanya ziwe na mafanikio mazuri.

Uongozi umesema kuwa kujenga mtu ni jambo kubwa linalotakiwa kufanywa kwa nguvu zote, kupitia kuweka mkazo katika sekta ya malezi ambayo huwa msingi wa sekta ya elimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: