Maahadi ya Quráni tukufu/ tawi la Bagdad inafanya nadwa ya Quráni

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Bagdad chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya nadwa ya Quráni chini ya anuani isemayo: (Manhaji ya Quráni katika kubainisha uhalisi wa utume.. Mtume wa mwisho kama mfano).

Nadwa imefanywa katika msikiti na Husseiniyya ya Hajat Fahariyya Biramani kwenye kitongoji cha Shaábu kaskazini mashariki ya Bagdad, mtoa mada alikuwa ni Ustadh Ahmadi Khaqani na kuhudhuriwa na kundi la waumini na wadau wa Quráni, pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Tambua kuwa tawi la Maahadi ya Quráni katika mji mkuu wa Bagdad, hufanya nadwa mara nyingi na harakati mbalimbali zinazo husu Quráni kwa lengo la kueneza uwelewa wa Quráni katika jamii.

Kumbuka kuwa nadwa hii ni miongoni mwa harakati za Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, zinazo fanywa na maahadi hiyo kwa lengo ya kueneza utamaduni wa Quráni katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: