Kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu amesema: Katika kuwatendea haki wanachuoni wetu tunatakiwa kuhuisha athari zao kadri ya uwezo wetu

Maoni katika picha
Toleo la kwanza la jarida la (turathi za Karbala za nakala-kale), linalotolewa na kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, ujumbe maridhawa wa Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi huu hapa:

Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu atoshae na rehema na amaini ziwe juu ya Muhammad na Aali wake watukufu, hakika kilicho fanywa na wanachuoni katika elimu nyingi na fani tofauti ni fahari inayotakiwa kuheshimiwa na kutukuzwa, historia inatuonyesha uhalisia wa tunayo sema, kwa masikitiko makubwa baadhi ya kazi zao zimetelekezwa.

Watu hao watukufu walitumia uhai wao kwa kusoma, kuandika na kufundisha, walikusanya karatasi moja baada ya nyingine, huku wakizungumza maneno mazuri na kutoa dalili katika maneno ya Mwenyezi Mungu au tafsiri na hadithi za Ahlulbait watakasifu (a.s).

Kati ya upungufu na ukamilifu zikapatikana tafiti za kielimu na kutengenezwa kanuni za usulu, na kufanyiwa kazi kwa kina mambo ya kifiqhi, jamii za kiislamu zikawa zinapita katika harakati za kielimu zilizo asisiwa na hao watu wema, Najafu, Hilla, Karbala na miji mingine.

Mji mtukufu wa Karbala ulikuwa na nafasi kubwa katika ulimwengu wa elimu kwa kipindi cha karne mbili au zaidi, pindi wasomi wakubwa walipo hamia katika mji huo na kuishi jirani na bwana wa mashahidi –a.s-, yawezekana kuwasiri katika mji huo kwa Wahidi Bahabahani ndio kulikowasha mwanga wa usomi na utafiti kwa kiasi kikubwa, na kundi kubwa la wanafunzi likanufaika nae na kuendelea kuwa chini ya malezi ya Marjaiyya baada yake.

Katika ikhlasi na uaminifu wetu kwa kundi la wanachuoni wema waliotangulia tunatakiwa kuhuisha athari zao kwa kiasi tutakacho weza, na kuziweka katika mazingira bora ya kutumiwa na wanafunzi wa dini, ukizingatia kuwa tafiti za kielimu kwa sasa zipo katika kipindi cha dhahabu, na kawaida ya tafiti ni kuonyesha mitazamo ya kielimu, utaipata wapi kama ikiwa imefungiwa katika nakala-kale na hakuna uwezekano wa kuzifikia?

Kwa hiyo ni jambo muhimu sana baada ya kuzihakiki tafiti ziandikwe katika mfumo wa majarida, ili iwe rahisi kusomwa na kila mtu, na kupatikana kwa wepesi na kusaidia kuonyesha turathi za Karbala za miaka tuliyo taja na baada yake.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awape nguvu watumishi wa idara hii muhimu, kwa kufanya tafiti adhim zitakazo fichua harakati za kielimu na kuziendeleza kulingana na hali ya sasa ambayo ni muhimu sana katika sekta ya historia.

Mwenyezi Mungu yupo nyumba ya makusudio.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: