Makumbusho ya Alkafeel na kamati ya athari na turathi zimejadili kuhusu kuwa na ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha makumbusho ya Alkafeel Ustadh Swadiq Laazim Zaidi pamoja na rais wa kamati kuu ya athari na turathi Dokta Liith Majidi, wamejadili kuhusu uwezekano wa kushirikiana katika mambo yanayo husu makumbusho, na upatikanaji wa vifaa-kazi vinavyo weza kuboresha sekta hiyo.

Bwana Zaidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika ziara hii ambayo ni miongoni mwa mfululizo wa ziara nyingi zinazo fanywa na idara ya makumbusho, kwa ajili ya kuweka ushirikiano na taasisi mbalimbali za makumbusho ili kubadilishana uzowefu, na kuangalia utendaji wa wengine katika sekta ya makumbusho, sambamba na kuitambulisha makumbusho ya Alkafeel na mali-kale ilizo nazo, na utendaji wake pamoja na njia za kutunza mali-kale, na harakati zingine zinazo fanywa na makumbusho hiyo, kama vile kuendesha semina, warsha na makongamano ya kielimu, rais wa kamati amefurahishwa na ziara hii na ameonyesha kuwa kamati anayo ongoza ikotayali kushirikiana na makumbusho ya Alkafeel katika mambo ya makumbusho, ili kuboresha utengaji wao, hali kadhalika tumewapa mualiko wa kutembelea makumbusho”.

Dokta Liith rais wa kamati amesema kuwa: “Kikao chetu kimejadili namna ya ushirikiano bora wenye manufaa kwa pande zote mbili, hususan namna ya kutunza na kuhifadhi mali-kale na ushirikiano katika sekta ya elimu kati ya kamati kuu ya athari na turathi pamoja na makumbusho ya Alkafeel, bila kusahau swala la faharasi na kuwasiliana na makumbusho kuu ya Iraq kwenye jambo hilo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: