Makamo rais wa chuo Dokta Nawaal Almayali amesema kuwa: “Chuo kimesha kamilisha maandalizi yote, ya kupokea wanafunzi waliokubaliwa katika ofisi za chuo zilizopo Najafu/ mtaa wa Nidaa nguzo namba 23/ jirani na jengo la makazi Amiraat”.
Akasisitiza kuwa: “Wanafunzi wanatakiwa kuja na vielelezo vinavyo hitajika ambavyo ni:
- 1- Kitambulisho cha uraia au cheti cha kuzaliwa (nakala halisi na kopi 1).
- 2- Kitambulisho cha uraia au cheti cha kuzaliwa cha mzazi (nakala halisi na kopi 1).
- 3- Kitambulisho cha makazi (nakala halisi na kopi 1).
- 4- Cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari (uthibitisho).
- 5- Kodi ya kukubaliwa kwake.
- 6- Picha binafsi ndogo (6).
- 7- Cheti cha daktari (kutoka kituo cha afya katika mji anaoishi mwanafunzi).
- 8- Ada ya masomo”.
Akamaliza kwa kusema: “Kitengo cha usajili kinafanya kazi siku zote za wiki ispokua Ijumaa, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni”.