Kikao cha wawakilishi wa mawakibu na idara za Husseiniyya

Maoni katika picha
Kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimefanya kikao pamoja na wawakilishi wa mawakibu Husseiniyya na idara zinazo fungamana nao kutoka mikoa tofauti, ndani ya ukumbi wa Qassim (a.s) katika Atabatu Abbasiyya na kuhudhuriwa na makamo katibu mkuu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi na mjumbe wa kamati kuu Sayyid Mustwafa Dhiyaau-Dini pamoja na rais wa kitengo hicho bwana Riyadhu Ni’mah Salmaan.

Kikao hiki ni muendelezo wa vikao vikubwa vilivyo fanywa mwaka jana, vinavyo lenga kuboresha utendaji wa vikundi hivyo kiidara.

Kwa mujibu wa maelezo ya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan kwa mtandao wa Alkafeel, amesema: “Kikao kimehudhuriwa na zaidi ya wajumbe (30), umewasilishwa utekelezwaji wa maazimio yaliyo pitishwa kwenye vikao vya nyuma, kwa mfano utengenezaji wa vitambulisho vipya na kuandaa ukurasa maalum wa maelezo, sambamba na kutolea maelezo changamoto wanazo pata wawakilishi wa mawakibu na vikundi vya husseiniyya na kujadili namna ya kutatua changamoto hizo”.

Akaongeza kuwa: “Tumekubaliana mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kufanya vikao kila baada ya miezi mitatu, na kuangalia mambo yaliyo tekelezwa baada ya kila kikao, pamoja na kuandika maoni yote, mahitaji na changamoto zilizo zungumzwa kwenye kikao hiki, kwa ajili ya kuwasilishwa kwa wahusika ili kutafuta utatuzi na kuondoa vikwazo vya utekelezaji wa jambo lolote lililo jadiliwa na kupitishwa kwenye kikao, katika kutumikia mambo ya Husseiniyya”.

Akamaliza kwa kusema: “Washiriki wametoa ushirikiano mzuri na wameomba vikao kama hivi viendelee kama tulivyo kubaliana”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: